Ticker

6/recent/ticker-posts

JINSI YA KUTENGENEZA JUISI YA MATUNDA MBALIMBALI

Image result for JINSI YA KUANDAA JUISI EMBE


MAHITAJI
450 grams Nanasi
 50 grams Tangawizi fresh osha vizuri menya
1 Carrot, chop chop
Ice cubes
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPO CHINI
Muda wa maandalizi : Dakika 15 
Muda wa mapishi : Dakika 15
Idadi ya wanywaji : watu 2
Tunda la nanasi na carrot vinachangia sana sukari yote ambayo uisi inatakiwa iwenayo. Tangawizi inaweka uwiano sawa wa ladha kati ya nanasi na karoti. Kama sio mpenzi wa Tangawizi sio lazima kuitumia, pia kama ni mpenzi wa nanasi au karoti unaweza zidisha kimoja wapo ili upate ladha halisi ya unachokipenda.
Tangawizi: Inategemea na ubora wa tangawizi, unaweza kuhitaji nyingi zaidi au wastani chamsingi uweze pata harufu mwanana katika juisi yako {aroma}.

Menya vizuri nanansi yako kisha katakata vipande vidogo

Chukua vipande vya nanasi, carrot na tangawizi kisha saga kwenye blenda au food processor (au juicer).

Saga vizuri kisha chuja vizuri.

Baada ya kuchuja kama haijachujika vizuri basi ongeza maji baridi na safi kiasi tu kisha chuja tena na kisha utapata juisi safi kabisa laini

Mpatie mnywaji ikiwa ya baridi weka na ice cubes. Kinywaji safi kabisa kwa majira ya joto yanayokuja hivi karibuni. A refreshing drink for the summer. Waandalie familia yako waweze kufurahia na nakujawengea tabia ya kuzoea kunywa maji.

Post a Comment

0 Comments