Ticker

6/recent/ticker-posts

UFUGAJI BORA SAMAKI AINA YA SATO


1.0 UFUGAJI WA SAMAKI
Ø  Ni kitendo cha kuzalisha samaki katika mabwawa, matenki au  Mifereji kwa lengo la chakula au kujipatia kipato

1.1 UMUHIMU WA UFUGAJI WA SAMAKI
Ufugaji wa samaki unazo faida mbalimbali ambazo ni:-
Ø  Kujipatia chakula bora na cha kutosha kwa ajiri ya familia na jamii.
Ø  Njia bora ya kujiajiri na kujiongezea kipato kutokana na mauzo ya samaki.
Ø  Hutoa fursa ya matumizi ya ardhi isiyofaa kwa ajili ya kilimo.
Ø  Ufugaji wa samaki hutoa nafasi ya kilimo mseto cha samaki na mazao/mifugo kwa wakati mmoja katika eneo moja, hivyo kutoa mavuno mengi.

1.2.0  MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA UFUGAJI WA SAMAKI;
1.2.1Mtaji
Ø  Mkulima anashauriwa kuhakikisha kuwa ana mtaji kabla hajaamua kufanya ufugaji wa samaki, kiwango cha mtaji kitategemea ukubwa wa mradi husika.
1.2.2        Soko
Ø  Ni vyema kujua upatikanaji wa soko pamoja na washindani wako kabla ya kuanzisha shughuli hii, japo kwa nchi yetu soko la samaki ni kubwa sana, hii inatokana na uhitaji mkubwa wa samaki katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
1.2.3        Elimu
Ø  Mkulima anapaswa kuwa na elimu ya kutosha  kuhusu samaki na jinsi ya kufuga ili aweze kuendesha mradi kwa urahisi, hivyo mkulima anaweza kutafuta mtaalam kutoka vyuo vya serikali au binafsi.
1.2.4        Upatikanaji wa mbegu(vifaranga) pamoja na chakula.
Ø  Mkulima anashauriwa kuwa na uhakika wa upatikanaji wa mbegu bora na chakula cha kutosha kwa ajili ya kulisha samaki.
1.2.5        Eneo la kufugia samaki
Ø  Ni vyema pia kutafuta eneo zuri kwa ajili ya kuchimba bwawa la kufugia samaki kwa kuzingatia upatikanaji wa maji kwa wakati wote wa msimu wa ufugaji, aina ya udongo, usalama na upatikanaji wa miundombinu husika (barabara, nishati ya umeme).

2.0       AINA YA SAMAKI;
2.1       Utafiti umefanyika katika nchi nyingi na kuonelea kuwa samaki aina ya perege/ngege/sato [tilapia] anafaa kufugwa katika mabwawakulinganisha na aina nyingine.       
2.2       Samaki wa aina hii wana sifa nzuri sana kwani; huishi kwenye maji yenye joto la kadri katika nchi nyingi, wanaweza kuzaana kwa wingi katika mabwawa, hula majani na chakula kingine chochote kinachopatikana kwa urahisi shambani au nyumbani, hukua kwa haraka, uvumilia sana changamoto za bwawa hii ikiwa ni  mabadiliko ya joto, hewa ya oksijeni, na pH, pia nyama ya samaki hawa ni tamu  na yenye ladha nzuri.
2.3       Kuna aina nyingi za sato(tilapia) kama vile Sato mwekundu, Sato wa Msumbiji, Sato mweupe na Sato wa Mwanza.                                                                                      
            Sato hawa hula mimea na majani, huhitaji chakula kingi na huzaana sana, wana doa moja kubwa kwenye pezi la   mgongoni. Sato hawa hula vijimea vya plankiton, hukua kwa haraka na wana mistari kwenye mikia. Aina nyingine za samaki zimechanganyikana na kuwa machotara hivyo siyo rahisi kuwatambua.
2.4       Sato wa  Mwanza ni moja kati ya aina ya tilapia inayoshairiwa kufugwa na wataalamu wengi kwa kuzingatia sifa mbalimbali tofauti na aina nyingine.

3.0    ENEO LINALOFAA KWA UFUGAJI WA SAMAKI AINA YA SATO:
3.1.1 Upatikanaji wa maji
3.1.1 Maji ni moja ya hitaji muhimu katika ufugaji wa samaki. Eneo litafaa kwa ufugaji wa samaki ni lenye maji ya kutosha kuendesha shughuli zote za ufugaji kwa kipindi husika.
3.1.2 Chanzo cha maji kwenye bwawa kinaweza kuwa; mto, mfereji wa kumwagilia, au chemi chemi. Bwawa linahitaji maji mengi na sio rahisi kujazwa na ndoo. Ili kuhakikisha kuwa bwawa linakuwa na maji ya kutosha muda wote, chanzo cha maji cha faa kuwa cha kuaminika.
3.1.3 Kama mkulima ana maji ya kujaza kwenye bwawa kwa msimu, inawezekana pia kufuga samaki. Lakini mkulima ahakikishe anapanda vifaranga vya samaki mwanzo wa msimu wa maji. Hii itatoa fursa kwa samaki kukua hadi kufikia kiwango cha kuvunwa kabla ya maji kukauka.
3.1.4 Kama wakulima wanatumia chanzo kimoja cha maji ni muhimu kuanzisha utaratibu ambao utawezesha wakulima wote kutumia maji hayo bila matatizo. Wafugaji wa samaki wanaweza kujaza mabwawa wakati wowote kutegemea ni kipindi gani maji hayatumiki sana kwa matumizi mengine.
3.1.5 Ili kuhakikisha kwamba bwawa halitumii maji mengi, ni muhimu kuimarisha kingo za bwawa kwa kushindilia vizuri udongo wakati wa ujenzi wa msingi wa bwawa. Hii ina maana kwamba udongo lazima uwe na kiwango kikubwa cha mfinyanzi. Udongo ambao unatumika kutengenezea vyungu au kufyatulia matofali ni mzuri sana kwa shughuli hii. Kama udongo hauna ufinyanzi wa kutosha bwawa litapoteza maji kwa urahisi na italazimu kuongezwa kwa maji mara kwa mara.
3.2 Aina ya udongo
3.2.1 Inashauriwa kuwa udongo wa tifutifu au mchanganyiko wa tifutifu na mfinyanzi ambao una uwezo wa kuhifadhi maji kwa muda mrefu unafaa zaidi kwa ufugaji wa samaki.
3.2.2 Udongo wa kichanga sio mzuri katika kushikilia maji lakini eneo lenye udongo wa aina hii linaweza kutumika kufuga samaki ikiwa mbinu mbalimbali zitatumika.
Zingatia
·         Kwa eneo lenye kichanga lakini lina upatikanaji wa maji ya kutosha mkulima anaweza kutumia mbinu ya kujaza mchanga kwenye mifuko ya saruji iliyokwisha kutumika na kuipanga kwenye kingo za bwawa ili kuimalisha kuta za bwawa. Kwakuwa mifuko inaweza kuoza kutokana na maji, inashauriwa ibadilishwe endapo kingo za bwawa zitaanza kumomonyoka na kuongeza tope ndani ya bwawa.
·         Karatasi ngumu ya nailoni yaweza pia kutumika kuzuia kupotea kwa maji na kulinda kingo za bwawa kumomonyoka.
·         Ujenzi wa kuta za bwawa kwa mawe au bwawa zima ni njia bora zaidi japo ni gharama ukilinganisha na mbinu nyingine.
Mifuko















Description: G:\DCIM\Camera\IMG_20140812_143017.jpg







picha ya bwawa liliotengeneza kwa karatasi ya nailoni

nylon
kuta
3.3  Mambo mengine ya kuzingatia katika uchaguzi wa eneo la kufugia samaki
3.3.1        Eneo liwe na mteremko kiasi ili kusaidia shughuli nzima ya uingizaji na utoaji wa maji kwenye bwawa. Nguvu nyingi zitatumika kuchimba bwawa eneo lenye mwinuko mkali na ni vigumu kujaza au kutoa maji kwenye bwawa lililochimbwa eneo la tambarare
3.3.2        Eneo linatakiwa kuwa na miundombinu bora na lenye kufikika kwa urahisi ili kusaidia usafirishishaji wa mazao, vifaranga na mahitaji husika.
3.3.3        Eneo lisiwe na historia ya mafuriko, hii ni hatari kwa kuwa mafuliko yanaweza kuvunja kingo za bwawa hivyo kuhatarisha shughuli ya ufugaji.
3.3.4        Eneo lisiwe karibu na maeneo hatarishi kama vile viwanda, shughuli za kilimo zenye kutumia kemikali ili kuzuia madhara ya kikemikali.
3.3.5        Eneo liwe karibu na mmiliki ili kuimalisha ulinzi na urahisishaji wa uendeshaji wa shughuli za uzalishaji. 
7.0       VYANZO VYA MAJI KWA UFUGAJI WA SAMAKI;
7.1       Ni vyema mkulima kuchagua chanzo cha maji kinachofaa kulingana na mazingira yake pamoja na manufaa kwa mkulima.                                                                         
7.2       Unaweza kutumia maji ya kisima, chemichemi, ziwa, mto na bomba kwa kuzingatia sheria na taratibu husika.                                                                 
7.3       Matumizi ya maji ya bomba katika ufugaji samaki ni lazima uzingatie ushauri wa kitaalamu. Lakini mambo yafuatayo yanaweza kumsaidia mkulima kutumia maji ya bomba kama chanzo cha maji; kabla ya kuweka samaki maji yawekwe kwenye bwawa kwa takribani siku kumi, hii itasaidia kuondoa chlorini kwenye maji, mbolea na tembe za vitamin c zaweza pia kutumika kuharakisha uondoaji wa chrolini katika maji.
7.4       Yote hapo juu yaweza kufanyika katika kuondoa chlorine kwenye maji lakini njia sahihi ni matumizi ya dawa maalumu aina ya ……………… inayopatikana madukani, japo ndani ya nchi yetu ni ngumu kuipata hivyo yaweza kuagiwa kutoka nje ya nchi.
8.0    GHARAMA ZA UCHIMBAJI WA BWAWA:
8.3    Gharama za uchimbaji zaweza kuainishwa katika makundi matatu; ushauri kutoka kwa wataalamu, gharama za uchimbaji na gharama za kuandaa bwawa kabla ya kuweka maji na wakati wa kuweka maji.
8.4    Gharama za uchimbaji wa bwawa zinatofautiana eneo kwa eneo na namna bwawa linavyochimbwa, hii ikihusisha nguvu na vifaa vitakavyotumika.
8.2    Ni vyema kuajiri watu kuchimba bwawa kuliko kutumia vifaa kama excavator, kama bwawa ni kubwa sana waweza kutumia vyote kwa pamoja. Bwawa linahitaji malekebisho mengi sana madogo madogo, hivyo matumizi ya watu kama nguvu kazi katika kuyafanya hayo ni muhimu.

4.0    KUSAFISHA ENEO, UCHIMBAJI WA BWAWA
4.1    Mara eneo linapochaguliwa, ni muhimu kuondoa majani, vichaka na miti yote. Mizizi ing’olewe kabisa kwa kuwa itaoza na kuacha mashimo ambayo yatasababisha maji kuvuja.
5.5    Mara eneo likisafishwa, bwawa lichimbwe kwa vipimo sahihi ili kujua ukubwa wa bwawa. Hii itasaidia katika uchimbaji, kujua ukubwa wa bwawa na idadi ya vifaranga watakao pandikizwa. Ni vyema kutumia kamba ili kunyoosha ukuta wa bwawa wakati wa uchimbaji.
4.3    Matuta yajengwe kwenye eneo lililosafishwa vizuri na ambalo halina mimea wala mawe kwa ajili ya kuzuia kupotea kwa maji. Pia udongo wa juu ambao una majani na mizizi usitumike kwa kutengenezea matuta ya bwawa.
4.4    Matuta yasijegwe katika eneo la kichuguu kuzuia kupotea kwa maji, japo ni vigumu na mara nyingine haiwezekani kabisa kuzuia uvujaji wa maji kwa aina hii.
8.2    Ni muhimu kuhakikisha kwamba matuta yanajishikilia vizuri kwenye ardhi. Hii inaweza kufanyika kwa kuchimba mfereji kuzunguka bwawa katikati ya eneo ambalo matuta yatajengwa.
4.2    Matuta lazima yashindiliwe vizuri kuzuia maji yasivuje. Njia rahisi ni kushindilia matuta kila baada ya kuweka sentimeta 30 za udongo. Hakikisha udongo unaloweshwa na kushindiliwa kwa kutumia kifaa chenye ubapa chini au kipande cha mti. Ushindiliaji wa aina hii ni sawa sawa na ushindiliaji wa sakafu ya nyumba. Ushindiliaji unafanya matuta kuwa imara na kutuamisha maji
4.0    Upana wa tuta la bwawa inategemeana na ukubwa wa bwawa,ni vyema uwe na mita 3 chini na mita 2 juu, mteremko(slope) katika ukuta wa bwawa ni kitu cha muhimu, hii ni kupunguza mmomonyoko,na inamrahisishia mhusika kuingia ndani ya bwawa kwa urahisi.
6.0    Kina cha bwawa ni vyema kitofautiane, hii ikiwa ni futi 3-4 sehemu ya kina kirefu na futi 1-1.5 sehemu ya kina kifupi. Eneo la kati lichimbwe katika namna itakayowezesha kupata slope ya bwawa katika utofauti wa kina cha juu na chini.
Description: G:\DCIM\Camera\IMG_20140526_163138.jpg
10.1  Bwawa likiwa na kina kifupi, itakuwa rahisi kwa maadui a samaki kukamata samaki. Pia bwawa likiwa na kina kifupi litapata joto haraka wakati wa mchana na kupoa haraka wakati wa usiku. Kwa hali hiyo joto la maji litabadilika sana kitu ambacho ni hatari kwa samaki katika bwawa
10.2  Sababu nyingine  ya kuwa na kina kinachostahili ni kwamba kwenye mabwawa yenye kina kifupi majani huota kwa kasi. Mimea kwenye bwawa la samaki ina athari sawa sawa na mimea shambani.
10.3  Wataalamu hawashauri kuchimba bwawa la kina kirefu kwa kuwa ni gharama, ngumu kulihudumia na kuvuna samaki…………
5.5    Urefu wa matuta utategemea wingi wa udongo, ukubwa wa bwawa na mfumo wa uvunaji wa samaki.
8.3    Ni muhimu pia bwawa lijengwe katika namna itakayoruhsu kujazwa na kukaushwa kwa maji kila inapohitajika. Hii ina maana kuwa maji yaingie bwawani sehemu iliyoinuka na yaweze kutolewa wakati wa kukausha kupitia sehemu ya chini ya bwawa.
5.4    Ili maji yafike sehemu ya bwawa iliyoinuka, mfereji wa kuchepushia maji kutoka kwenye
kijito utengenezwe.
5,3    Sehemu ya kuingiza maji iwekwe kwenye kina kifupi na ile ya kutolea maji iwekwe kwenye kina kirefu kwa kuzingatia picha hapo chini.

Post a Comment

0 Comments