Ticker

6/recent/ticker-posts

JINSI YA KUTENGENEZA CHAKI UKIWA PEKE YAKO NYUMBANI

Image result for CHALKS


Hujambo mpenzi msomaji na KARIBU Sana katika Blogu yako pendwa....
Leo kama kichwa cha habari kinavyoonesha hapo juu tutajifunza jinsi ya kutengeneza chaki za aina zote.
Tofauti ya chaki inatokana na malighafi inayotumika kutengenezea chaki husika mfano rangi na aina ya chokaa inayotumika.


MARIGHAFI;

1.CHOKAA NYEUPE.

2.MAJI

3.RANGI(Kama unahitaji iwe ya rangi)

4.FOIL PAPER(MAUMBO)

5.MOTO


HATUA YA KWANZA 
Chukua chokaa kilo moja iliyochekechwa na kupata unga ulio safi,maji lita moja,rangi 10mls.Changanya mchanganyiko huu kwa pamoja upate uji mzito na ukoroge kwa dakika kumi na tano.

HATUA YA PILI. 
Weka mchanganyiko wako katika maumbo yako ya vibox au bati ambazo zimekatwa katika shape unayoitaka.
Weka juani chaki zako mpaka zikauke.
Zitoe kwenye maumbo uziweke jikoni na kuzichoma kama unavyochoma matofari au vyungu mpaka ukiishika uone inatoa vumbi na ukiidondosha ikatike vipande viwili au zaidi.
CHAKI ZAKO TAYARI PAKI NA KUZIPELEKA SOKONI


JIfunze zaidi kupitia video hii hapa





usiache kukoment na kusubscribe

Post a Comment

0 Comments