Ticker

6/recent/ticker-posts

JIFUNZE KUPIKA KEKI YA NUSU KILO

May be an image of cake
 
Vinavyohitajika
· Siagi ya baking 250g – robo kilo.
· Sukari 250g – robo kilo.
· Unga wa ngano 500g –nusu kilo.
· vanilla kijiko 1 cha kulia chakula.
· Baking powder kijiko 1 cha kulia
· Mayai 6-8
JINSI YA KUTAYARISHA
· Weka siagi ndani ya bakuli la kuchanganyia pamoja na sukari uichanganye pamoja mpaka vichanganyike vizuri (unaweza kuisaga sukari yako ukitaka lakini si lazima).
· Ikichanganyika vizuri weka yai moja moja uchanganye pamoja pia ichanganyike vizuri.
· anza kuweka unga kwenye mchanganyiko wako Hakikisha unaweka unga wako kidogo kidogo alafu unachanganya na sio wote kwa wakati mmoja.
.weka vanila kijiko kimoja na uchanganye kidogo
. weka baking poda yako na uchanganye
Baada ya hapo mchanganyiko wako utakua tayari kwa kuokwa..
ZINGATIA
Unaweza kutumia mashine ya kusagia keki na kama huna tumia mwiko tu kwa kuchanganyia na itakuwa nzuri tu usikhofu.

Post a Comment

0 Comments